Ligi kuu ya soka Tanzania Bara kesho Jumamosi Oktoba 29, itaendelea tena ikiwa ni mzunguuko wa wa 13 tangu msimu huu wa 2016/17 ulipoanza rasmi Agosti 20 mwaka huu.

Kikosi cha Toto Africans ya Mwanza kesho kitapambana na wakata miwa kutoka Manungu, Turiani mkoani Morogoro (Mtibwa Sugar) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City ya Mbeya ambao watakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mwadui ya Shinyanga inatarajiwa kuialika Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu na Ndanda zitachuana Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Keshokutwa Jumapili Oktoba 30, 2016 Young Africans itacheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru huku Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

LA Galaxy Yamnyatia Rooney, Yajizatiti Kumlipa Mshahara Mnono
Lucas Perez Kuikosa Sunderland