Mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi huenda akasalia jijini London, kufuatia uongozi wa klabu ya West ham Utd kuonyesha dhamira ya kumsajili.

The Hammers wamedhamiria kumbakisha jijini London mshambukliaji huyo kutoka nchini Ublegiji, kwa kuandaa kitita cha Pauni milioni 31, ambacho wanaamini kitatosha kutimiza mpango wa kumuhamishia London Stadium.

Batshuayi mwenye umri wa miaka 23 amekua na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea, hali ambayo inatoa msukumo kwa viongozi wa The Blues kujifirikia kumuweka sokoni kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 33 itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Meneja wa West Ham Utd, Slaven Bilic anaamini uwezo wa mshambuliaji huyo utafanikisha mipango yake ya msimu ujao, baada ya msimu huu kwenda mrama.

Batshuayi alijiunga na Chelsea akitokea Olympic Marseille ya Ufaransa mwanzoni mwa msimu huu kwa matarajio makubwa ya kupelekea upinzani katika kikosi cha kwanza cha The blues, lakini mambo yamekua tofauti, kwani mpaka sasa ameshacheza michezo 16 ya ligi ya England.

Ozil, Draxler, Gomez Kuikosa England
Mkwasa: Tulitarajia Kupangwa Na Timu Yoyote