Vinara wa ligi kuu ays oka nchini England (Chelsea), wamepanga kumtema mshambuliaji wao kutoka nchini Ubelgiji Michy Batshuayi itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Gazeti la The Daily Mirror limeripoti kuwa, meneja wa Chelsea Antonio Conte ameonyesha utayari wa kuona mshambuliaji huyo anaondoka mwishoni mwa msimu huu, bila kujali gharama kubwa iliyotumika kwa ajili ya usajili wake mwanzoni mwa msimu huu.

Batshuayi, mwenye umri wa miaka 23, alisajiliwa na The Blues akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Olympique Marseille kwa ada ya Pauni milioni 33.

Mpaka sasa ameshindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha The Blues, hali ambayo inaendelea kumpa msukumo Antonio Conte kumruhusu aondoke.

Conte amekua akishindwa kumtumia Batshuayi, hata inapotokea mshambuliaji Diego Costa akiwa majeruhi.

Tangu mwanzoni mwa msimu huu Batshuayi, amecheza michezo 16 akitumika kama mchezaji wa akiba na mara tano akicheza katika kikosi cha kwanza.

Ameshafunga mabao matano katika michezo 21 aliyocheza, takwimu ambazo haziendeni na thamani ya pesa iliyotumika kumsajili akitokea Ufaransa.

Ndoto Za Wayne Rooney Zamtesa Ronald Koeman
Operesheni kamata viroba yaanza Dar es salaam