Msanii maarufu nchini Marekani, Kanye West ametua barani Afrika ambapo kwasasa yupo tayari nchini Uganda kwa ajili ya kupata midundo tofauti tofauti kutoka Afrika ili aweze kukamilisha albamu yake ya Yadhi inayotarajiwa kuachiwa rasmi mwezi November mwaka huu.

Kanye West alifurahishwa na kupenda mdundo wa Immediately uliotayarishwa na Mystro kutoka Nigeria akiwa amemshirikisha Wizkid kwenye ngoma hiyo. wakiwa nchini humo mpaka sasa wameshafungua studio ndogo na tayari wameshaanza kurecord.

TMZ ilishawahi kufanya mahojiano na rapper huyo na akaeleza mpango wake wa kutembelea bara la Afrika kutaka kupata radha tofauti ya muziki ikiwemo kugundua uhalisia wa Afrika na jinsi ambavyo wana andaa muziki

Hata hivyo, Kanye West amesema kuwa anataka kuimalizia albamu yake hiyo akiwa mahali ambapo watoto wake wanaweza kuwa pamoja naye.

Atakayempata Mo Dewji kupewa Sh1 bilioni
NEC yatangaza tarehe ya uchaguzi Serengeti na Simanjiro

Comments

comments