Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi amesema ipo changamoto ya kufanya baadhi ya maamuzi bila kuwa na Takwimu halisi hasa kwa mtu mmojammoja na kwamba ili kuepukana na tatizo hilo kuna haja ya kuimarisha mifumo ya ufahamu juu ya masuala ya kitakwimu.

Dkt. Katunzi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Dar24 ofisini kwake, juu ya mambo mbalimbali ya uimarishaji wa mifumo ya data kwa kufanya uzalishaji, na utumiaji wa takwimu za kilimo kuwa wa kisasa na kuadhimisha siku ya Takwimu za Afrika.

Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi.

Amesema, watu wengi hufikia kwamba Takwimu ni maamuzi ya Serikali kitu ambacho si sahihi kwani hata mtu mmoja mmoja anaweza kuwa na takwimu ambazo zinaweza kumsaidia katika kufanikisha mambo yake ya kila siku ikiwemo kuimarisha njia zake za kiuchumi.

“Mfano Mkulima anahitaji kujua takwimu za masoko ya kibiashara, ajue takwimu za usafirishaji wa mazao, ajue takwimu za bei ya mazao na taarifa hizi kwa mkulima zitamsaidia sana kufanya maamuzi ya wapi auze mazao yake na ni kwa wakati gani.” amefafanua Dkt. Katunzi.

Sehemu ya Washiriki katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.

Aidha ameongeza kuwa, mfumo wa takwimu upo katika mpagilio halisi wa kukusanywa, kuchakatwa na kusambazwa katika mfumo wa utambuzi ni wapi zinapelekwa na ni nani anayekwenda kuzitumia ili iwe rahisi kwake kufanikisha malengo yake kulingana na uhitaji kwa kuzielewa na kuzitumia.

Katika kilele hicho cha siku ya Takwimu za Afrika, mada mbalimbali zilijadiliwa, ikiwemo kuarifu sera kwa nia ya kuboresha ustahimilivu katika kilimo, lishe na usalama wa chakula barani Afrika.

Serikali kuboresha mashamba yake ya Mifugo
Sony Music wamuibua Aslay mafichoni