Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Dkt Fred Matiang’i amesema mwanasiasa wa upinzani aliyetimuliwa nchini humo Miguna Miguna hatoruhusiwa kuingia nchini Kenya mpaka pale atakapoomba uraia wa nchi hiyo.

Amesema mwanasiasa na mwanaharakati huyo, alipoteza uraia wake tangu mwaka 1998 pindi alipochukua uraia wa Canada kwani sheria ya Kenya hairuhusu mtu yeyote kuwa na uraia wa nchi mbili licha ya kuwa Miguna alizaliwa nchini Kenya.

Dkt Matiang’i, amezungumza hayo pindi alipokuwa akihojiwa na kamati ya bunge, amesema mwanasiasa huyo ambaye pia ni wakili alijipatia paspoti yake ya Kenya na kitambulisho cha taifa anachokitumia kwa sasa kwa njia ya ulaghai.

“Yeyote aliyechukua uraia wa taifa jingine kabla ya katiba ya sasa kuidhinishwa mwaka 2010 ambaye anafikiri kwamba ataweza kurejea bila kufuata utaratibu uliowekwa anajihadaa.

“Hapana shaka kwamba Miguna alizaliwa Kenya.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa katiba ya kabla ya 2010, yeyote aliyechukua uraia wa nchi nyingine alipoteza uraia wake wa Kenya  na  Bunge limeidhinisha sheria inayoeleza jinsi mtu kama huyo anavyoweza kuupata tena uraia wa mchi hiyo.

 

Amerika kusini waongoza kununua tiketi za kombe la dunia
Magufuli aishukia Tanesco, aagiza kushusha bei ya umeme

Comments

comments