Mwanasiasa wa upinzani aliyezuiwa kuingia Kenya wiki iliyopita na kusafirishwa kwa lazima hadi Dubai ameelekea nchini Canada, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.

Miguna Miguna, ambaye ni wakili, amesafiri kwa ndege iliyokuwa ikielekea Toronto, Canada, baada ya kukaa katika uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa siku nne.

Gazeti la Nation, limesema afisa mmoja wa serikali amewafahamisha kwamba, Miguna aliondoka Dubai akitumia ndege ya Air Canada 57 (ACA57) baada ya kuwasilisha pasipoti yake ya Canada.

Hatas hivyo, Miguna alikamatwa na polisi mara baada ya kumuapisha kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kuwa Rais wa Wananchi katika hafla iliyofanyika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi mnamo 30 Januari

 

 

Tanzia: Winnie Mandela afariki dunia
Watanzania watakiwa kuacha kulalamika

Comments

comments