Miili ya Wanajeshi nane wa Uganda waliouawa katika shambulio lililotekelezwa na kundi la Al shabaab imerejeshwa nyumbani na kukabidhiwa familia zao kwa ajili ya maziko.

Msemaji wa jeshi la Uganda (UPDF) amesema kuwa idadi ya wanajeshi wa Uganda waliouawa imeongezeka hadi nane, baada ya majeruhi wanne kufariki.

Jeshi la Uganda limesema kuwa zaidi ya wapiganaji 30 wa Al shabaab waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika siku ya Jumapili.

Naibu wa Kamanda wa majeshi ya nchi kavu Meja Jenerali, Sam Kavuma ndiye aliyepokea miili ya wanajeshi wanne waliofikishwa Jumanne kuwapongeza marehemu hao kwa kazi waliofanya.

“Hawakufa bure, wamefanya kazi nzuri. Wapewe pongezi, waliweza kuwazuia wanamgambo wa Al shaabab wasifanye mashambulizi yao na kuwaangamiza.”amesema Kamanda Kavuma.

Sababu za mwanamke kufyatulia risasi ofisi za YouTube zabainika
Serikali yamuomba Mdee kusaidia utatuzi mgogoro wa Ardhi