Malkia Elizabeth wa II leo ametoa hotuba kwa njia ya televisheni kuadhimisha miaka 75 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Maadhimisho hayo mwaka huu 2020 yamekuwa ya tofauti baada ya uwepo wa mlipuko wa homa kali ya mapafu Covid -19 uliofanya watu wasalie majumbani mwao.

Hotuba ya Malkia Elizabeth ni ishara muhimu inayotolewa miaka 75 tangu baba yake Mfalme George wa VI alipolihutubia taifa kwa njia ya redio na kutangaza ushindi katika vita kuu vya pili vya dunia.

Malkia amezungumzia mitaa ya Uingereza kuwa wazi bila watu kwa siku hii muhimu kwamba yeye anaona mitaa haipo wazi na hina upweke kwani imejaa upendo.

Matukio kadhaa yaliyopangwa kusherehekea siku ya ushindi wa majeshi ya nchi washirika dhidi ya manazi wa Ujerumani yamefutwa baada ya serikali kupiga marufuku ya mikusanyiko kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Hata hivyo tukio la kurushwa kwa ndege za kivita limefanyika kama kawaida.

Waziri Kabudi amesema hawana dawa za kugawa, utafiti kwanza
Wataalamu wa afya kuhudumia wananchi kwa simu saa 24