Meneja wa mabingwa wa Kombe La Chama Cha Soka England (FA Emirates CUP) Arsenal Mikel Arteta amewasiliana na kiungo wa FC Barcelona Ivan Rakitic akijaribu kumshawishi ajiunge na klabu hiyo ya jijini London.

Ripoti kutoka England zinaeleza kuwa, Rakitic amepewa ruhusa ya kuondoka FC Barcelona majira ya joto na amehusishwa na baadhi ya klabu za soka nchini humo ikiwepo Arsenal na Manchester United.

Arteta amekua meneja wa kwanza kutajwa kwenye mkakati wa kufanya mazungumzo na kiungo huyo kutoka Croatia, akiamini atamfaa katika kuboresha kikosi chake msimu ujao.

Mazungumzo aliyoyafanya Arteta na kiungo huyo amemueleza kuwa anatamani ajiunge na timu yake, huku akimueleza kuwa amedhamiria kurekebisha kikosi chake licha ya fedha finyu aliyopewa kwenye bajeti ya usajili.

Mkataba wa Rakitic na FC Barcelona unamalizika msimu ujao, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anatarajiwa kupatikana kwa bei nafuu.

Wilfred Zaha aiogopa mitandao ya kijamii
Makonda akabidhi ofisi Dar es Salaam