Serikali imesema kuwa mikataba ya madini iliyopo haitavunjwa licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya kisheria yaliyopitishwa na bunge mjini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi bungeni mjini Dodoma, amesema kuwa mikataba hiyo itakuwa ya mwisho kwani kuanzia sasa wawekezaji watakaokuja katika sekta hiyo watatumia leseni.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali itafanya marejeo ya mikataba hiyo iliyopo na kwamba taarifa ya mapitio hayo itatolewa na bunge.

“Sisi tungeendelea na mfumo huu wa mikataba ya bila kufanya mabadiliko, maana tungeivunja mikataba iliyopo,”amesema Prof. Kabudi.

Hata hivyo, Kampuni ya Acacia moja ya Kampuni za uchmbaji madini imefungua kesi ya kuomba upatanishi wa mgogoro baina yake na Serikali kuhusu zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.

Mwijage azikingia kifua bidhaa za ndani
Bunge la 11 lawapiga kitanzi watumishi Serikalini