Kiungo Mikel John Obi yupo tayari kuachana na klabu ya Chelsea itakapofika mwezi Januari mwaka 2017.

Gazeti la The Daily Star limeeleza kuwa, tayari kiungo huyo kutoka nchini Nigeria ameanza kusaka mahala pa kucheza soka lake, na amedhamiria kwenda nchini Ufaransa au China.

Obi ameingia katika mkakati wa kutaka kuihama The Blues, kufuatia mipango ya meneja mpya Antonio Conte kumuweka mbali na kikosi cha kwanza.

Jarida la michezo la nchini Ufaransa Le 10 Sport, nalo limeeleza kuwa, meneja wa klabu ya Olympic Marseille Rudi Garcia ameweka dhamira ya kumsajili Obi, kwa kuamini ataweza kukisaidia kikosi chake kwa msimu huu wa 2016/17.

Mahakama Kuu yabariki ushindi wa Bulaya, Wassira aanguka tena
JPM amteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi kuwa Katibu Tawala Kagera, Ampa shavu Jaji Warioba