Sanamu ya dhahabu ya mikono ya rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela imeuzwa kwa thamani ya $10 milioni kwa mfumo wa bitcoin.

Kampuni ya Canada inayofanya kazi ya kubadilisha fedha kwa njia ya mfumo wa ‘bitcoin’ imenunua sanamu hiyo kutoka kwa mfanyabiashara Malcolm Duncan.

Imesema kuwa lengo la kununua mikono hiyo ni kuanzisha ziara yenye kampeni maalum ya kuelimisha vijana kuhusu maisha ya Nelson na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Hii ni mara ya kwanza kwa kazi inayoakisi muonekano wa Mandela kuuzwa kwa mfumo wa bitcoin.

Mandela alifungwa jela miaka 27 kwa hatua yake ya kupinga utawala wa kikabulu wa Afrika Kusini. Aliachiwa huru mwaka 1990 ambapo alikuwa rais wa taifa hilo tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999 alipong’atuka kwa hiari.

Mzee Mandela alifariki dunia mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95. Heshima ya kazi aliyoifanya wakati wa uhai wake imefanya jina lake kuwa jina linalotumika kukuza na kuhamasisha katika sekta zote, ikiwa ni pamoja na biashara na kazi za sanaa.

Urusi yajibu mapigo ya Marekani, yawafukuza Wanadiplomasia 60
UKAWA waituhumu serikali kwa hujuma

Comments

comments