Mwimbaji wa Pop, Miley Cyrus amethibitisha kufunga ndoa na muigizaji maarufu wa Australia ambaye alikuwa mchumba wake wa muda mrefu, Liam Hemsworth.

Cyrus ameweka mtandaoni picha za sherehe za harusi hiyo ambayo imeelezwa kuwa ilifanyika Jumapili iliyopita. Wawili hao walikutana miaka kumi iliyopita walipokuwa wakishiriki filamu ya The Last Song.

Novemba mwaka huu walikumbwa na janga baada ya nyumba yao ya California kuteketea kwa moto. Imeelezwa kuwa sherehe za harusi yao zilifanyika katika nyumba nyingine ambayo inamilikiwa na Cyrus iliyoko Franklin, Tennessee.

Tukio la ndoa ya wawili hao ilihudhuriwa na watu wachache ambao ni familia pamoja na marafiki wa karibu pekee. Picha inayowaonesha wakiwa wamekumbatiana kama watu wanaotumia moyo mmoja iliweza kuzungumza zaidi.

Wasanii hao wamepitia vuguvugu la ndoa kwa kipindi kirefu, ambapo mwaka 2012 walilazimika kutengana lakini walianza kuonekana wakiwa pamoja tena mwaka 2015.

Novemba mwaka huu, Cyrus alieleza kuwa yeye na Hemsworth walifanikiwa kutoka wakiwa salama kwenye nyumba yao iliyoteketea kwa moto, hivyo walionesha kuwa walikuwa wanaishi pamoja.

Mipango ya mafanikio hufa katika hatua hii
Museveni aibua gumzo la Bebe Cool Vs Bobi Wine

Comments

comments