Milio ya risasi imesikika karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Burkina Faso kukiwa na uasi wa wanajeshi, Pia milio mingine ya risasi imesikika kwenye kambi kadhaa mjini Ouagadougou, huku wanajeshi wakishinikiza kufutwa kazi kwa wakuu wa jeshi na wakidai rasilimali zaidi za kusaidia mapambano dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu

Serikali imesema kuwa vurugu zimedhibitiwa na imetupilia mbali tetesi za kuwepo kwa jaribio la mapinduzi, ikiwa ni zaidi ya wiki moja baada ya wanajeshi 11 kukamatwa kwa madai ya kupanga mapinduzi.

Hivi karibuni kumekuwa na ishara ya kuongezeka kwa kutoridhika na serikali ya Rais Roch Kaboré kutokana na kushindwa kwake kukomesha uasi wa Kiislamu ambao umelitikisa taifa hilo la Afrika Magharibi tangu mwaka 2015.

Waandamanaji wanaounga mkono wanajeshi hao walichoma moto jengo la makao makuu ya chama tawala na kuendeleza Milio ya risasi katika kambi za kijeshi magharibi na kusini mwa mji mkuu, na katika kambi ya anga karibu na uwanja mkuu wa ndege.

Wanajeshi waliopatikana na hatia ya jaribio la mapinduzi mwaka 2015 wanazuiliwa katika kambi hiyo iliyoko magharibi mwa nchi inayojulikana kwa jina la Sangoule Lamizana.Milio ya risasi pia ilisikika katika kambi za kijeshi katika miji ya kaskazini ya Kaya na Ouahigouya, ubalozi wa Marekani umeeleza.

Taliban wataka kujua hatma yao
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 24, 2022