Marafiki wa milionea raia wa Zimbwabwe, Genius Kadungure maarufu kama Ginimbi, wamesema atazikwa na gunia lililojaa Dola.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Zimbabwe, mfanyabiashara huyo aliyeishi maisha ya kifahari aliacha maagizo hayo kwa wanachama wa “all-white funeral”.

Ginimbi alifariki kutokana na ajali ya gari Jumapili, jijini Harare pamoja na mlimbwende Mitchelle Amuli aliyejulikana kama Moana.

Familia ya Moana imetaka fedha za mazishi kutoka kwa wanaowafariji na imeahirisha mazishi kwa wiki mbili ikisubiria majibu ya DNA na kukusanya michango ya kifedha kwa ajili ya kumuaga kwa heshima.

Matajiri wa Zimbabwe wamekuwa wakiahidi fedha kwa ajili ya mazishi ya Ginimbi.

Naibu Waziri Tino Machakaire ameahidi kununua jeneza kubwa kwa ajili ya Ginimbi hulu Mbunge Temba Mliswa amechangia wanyama wengi kwa ajili ya kuchinjwa kwenye mazishi hayo.

Ginimbi na Maona walikuwa wanatoka kwenye sherere ya “all-white” ambapo gari yao iligongana na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao, ilichepuka nje ya barabara na kugonga mti kisha kulipuka moto.

Rais Magufuli amteua Majaliwa kuwa Waziri Mkuu
NBS: Mfumuko wa bei kuimarika