Kampuni ya kutengeneza roboti ya nchini Urusi inatafuta sura ya binadamu atakaye kubali kulipwa ili kuitumia kwenye  bidhaa yake mpya ‘Promobot’.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kampuni hiyo imesema kwamba iko tayari kulipa $200,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 460 za Kitanzania mtu atakaye kuwa tayari  kuipa kampuni hiyo haki ya kuutumia muonekano wa sura yake milele kwenye roboti hilo.

Kampuni hiyo imeweka wazi mpango wao, ambao ni kutumia roboti hiyo mpya yenye sura ya kibinadamu kama msaidizi katika maeneo yenye shughuli nyingi kama vile hoteli na maduka makubwa.

Kulingana na taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imepata mteja ambaye anatazamia kumuweka roboti huyo kama msaidizi katika viwanja vya ndege, maduka makubwa na maduka ya reja reja ifikapo mwaka 2023.

Wizkid atangazwa msanii bora wa mwaka Apple Music
Aliyeuza senene kwenye ndege kufikishwa Mahakamani