Aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezungumzia hatua ya Rais Dkt. John Magufuli kumuengua kwenye wadhifa wake akisema anakuwa mzuri anapotokea benchi.

Amesema kuwa kwa wale wanaomfahamu wanajua kazi yake akiwa anatokea benchi, huwa anakuwa mzuri zaidi na ndiye aliyeshiriki kubadilisha sera ya mafuta ya tozo ya Rea ambapo serikali ilikuwa inapoteza bilioni 600.

“Mimi wanaonijua, wanafahamu kazi yangu, nikiwa benchi ninakuwa mzuri zaidi, mimi ndiyo nilishiriki kubadilisha sera ya mafuta na tozo ya Rea ambapo Serikali ilikuwa inapoteza bilioni 600,” amesema Mwijage.

Aidha, Mwijage amesema kuwa waziri yeyote wakiwamo hao walioteuliwa akitaka ushirikiano yupo tayari kufanya hivyo, na kuongeza kuwa kitu anachokumbuka na alichokiacha kama alama ni kuwaelewesha Watanzania kuhusu dhamira ya kuwa na nchi ya viwanda, ambapo hivi sasa nchi nzima wanazungumza viwanda.

Hata hivyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja sababu ya kuwatumbua waliokuwa Mawaziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba, pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kuwa walishindwa kumaliza mgogoro wa zao la korosho, huku akiwapongeza kwa kuhudhuria hafla ya uapisho.

 

 

Video: Tundu Lissu amvaa tena Magufuli, Maagizo mazito, Mbwa wanasa shehena dawa za kulevya
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 13, 2018