Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba amesema kuwa yeye ni mmoja kati ya Watanzania wazalendo wanaounga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kutokana na harakati zake hizo, baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa wamemuundia vikundi na kuanza kumtishia maisha.

Amesema kuwa mpaka sasa amesharipoti kwenye vyombo vya dola ili viweze kuchukua hatua stahiki kwani kila binadamu ana haki ya kuishi.

“Kwanza kabisa mimi sipiganii CCM wala Chadema, sasa nawashangaa hawa viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa kuniundia vikundi na kuanza kuniwinda, wajue tu kwamba mimi nafanya hivi kuunga mkono yanayofanywa na Rais Dkt. Magufuli, sina muda wa kuzozana na mtu mwingine,”amesema Musiba

Hata hivyo, Musiba ameongeza kuwa kamwe hataacha kuunga mkono yanayofanywa na Rais Dkt. Magufuli kutokana na vitisho anavyovipata, hivyo ataendelea na harakati zake.

 

VIDEO: Samatta azungumzia ’’Hat Trick’’ aliyofunga hivi karibuni.
JPM amteua JK kumwakilisha sherehe za uapisho