Wakati Rais wa TFF, Wallace Karia akieleza kwamba hajui aliyerusha video ikimuonyesha amekwepa kusalimiana na kocha wa Geita Gold, Fred Felix Minziro, amesema video hiyo imetengenezwa kwa lengo la kumchonganisha na kiongozi huyo wa soka nchini.

Tukio hilo lilitokea wakati wa utoaji wa tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Daraja la Kwanza msimu huu 2020/21, baada ya mchezo wa fanali uliozikutanisha Geita Gold FC dhidi ya Mbeya Kwanza uliochezwa Jumapili (Mei 30), Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Minziro amesema: “Sijui aliyeiposti alikuwa na maana gani, muulize Minziro atakueleza ukweli,” amesema Karia.

Minziro alipoulizwa alisema ni video ambayo imetengenezwa kwa nia ovu ya kumchonganisha na Karia.

“Hivi Karia akatae kunipa mkono kwa sababu gani? ukiachana tu na kuwa rais wa mpira ni rafiki yangu na sijawahi kutofautiana naye, ni watu tu wameamua kuitengeneza kwa nia ovu ya kunichonganisha naye,” amesema.

Amesema alipokuwa jukwaani jana, Karia alimwambia ageuke ili apigwe picha na waandishi wa habari.

“Kama angekuwa ananichukia angeniambia hivyo?,” alihoji Minziro na kubainisha kwamba hata leo asubuhi ameongea na Karia.

“Sina ugomvi na Karia, ni rafiki yangu tangu nacheza mpira na hata leo asubuhi nimezungumza naye, ni watu tu wanatengeneza vitu vya ajabu ajabu ili kuchonganisha wengine,” amesema.

Amesema kama kuna mtu amemsema vibaya Karia baada ya kuangalia video ile basi amemuonea, kwa kuwa ni video ambayo anadai imetengenezwa ili ionekane Karia hakumpa mkono wakati si kweli.

Jaji Mtanzania achaguliwa kuongoza Mahakama ya Afrika
Mbunge atolewa Bungeni kisa mavazi