Majogoo wa jiji Liverpool, wamekubali ofa ya klabu ya Stoke City ambayo imemlenga kiungo kutoka nchini Wales, Joe Allen.

Liverpool wameripotiwa ofa hiyo inayokadiriwa kufikia Pauni Milioni 13 na inaamika watakuabili kumuachia, kutokana na Joe Allen kutokuwa sehemu ya mipango wa meneja wao kutoka nchini Ujerumani Jurgen Klopp.

Jambo lingine ambalo linatoa msukumo wa kuuzwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ni muda wa mkataba wake ambao umesaliwa na mwaka mmoja.

Joe Allen amekua kivutio kwa viongozi wa klabu ya Stoke City, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na timu yake ya taifa, katika fainali za Euro 2016 ambazo zilifikia tamati hivi karibuni nchini Ufaransa, ambapo Wales waishia katika hatua ya nusu fainali.

Klabu ya Swansea City, nayo inatajwa kuwa katika mbio za kutaka kumsajili Joe Allen, lakini ofa yao inasemekana haina nguvu kama ilivyo ya Stoke City ambao wamedharia kumng’oa kiuongo huyo Anfield.

Sam Allardyce Kumrudisha Ulingoni David Moyes
Panga lingine lafyeka mishahara wafanyakazi NSSF