Uongozi wa klabu ya Man Utd unajiandaa kuvunja mkataba wa kiungo kutoka nchini Ujerumani Bastian Schweinsteiger, ambaye bado hajafit kwenye mipango ya meneja Jose Mourinho.

Gazeti la The Sun la nchini England limeeleza kuwa, kiungo huyo wa zamani wa FC Bayern Munich ambaye analipwa mshahara wa Pauni laki moja na Themanini (180,000) kwa juma, huenda akalipwa Pauni milioni 18 kama fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wake ambao umesaliwa na muda wa miaka miwiwli.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo zililifikia gazeti la The Sun zinaeleza: “Bastian ni mchezaji ambaye anaonaka kukamilika katika kila hali, kutokana na nidhamu yake ya kufanya mazoezi kila kukicha.

“Amekua mtu wa kipekee na ana muonekano tofauti, licha ya kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Mourinho.

“United wana matumaini ya kuvunja mkataba wake, ili kutoa nafasi kwa kiungo huyu kuendelea na maisha yake ya soka mahala pengine.”

Katika hatua nyingine chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa, huenda Schweinsteiger akauzwa wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka 2017, na kama itakua hivyo atalipwa fidia ya Pauni milioni nne (4).

Wakala Wa Yaya Toure Kuzungumza Na Pep Guardiola
Magufuli avunja rekodi ya Lowassa, amfunika