Kiungo Samir Nasri amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester City ya England.

Kiungo huyo kutoka nchini Ufaransa amefanikisha hatua ya kuondoka Etihad Stadium, baada ya kukabiliwa na mtihani wa kujihakikishai nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza tangu msimu uliopita ambapo alicheza michezo 12 pekee.

Hata hivyo changamoto iliyokua inakabili Nasri kwa muda mrefu ni majeraha ya mara kwa mara, hali ambayo ilimsababishia kushindwa kuwa katika kiwango chake kama ilivyozoeleka.

Mchana wa leo Nasri alimilisha taratibu za kufanyiwa vipimo vya afya huko nchini Hispania na inaaminiwa uwepo wake katika kikosi cha Sevilla huenda ukamuwezesha kurudi kwenye kiwango cha kucheza soka la ushindani kama ilivyokua siku za nyuma.

Mwishoni mwa juma lililopita, meneja wa Man City Pep Guardiola, alimtumia Nasri kama mchezaji wa akiba wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya West Ham, ambao walikubali kibano cha mabao matatu kwa moja.

Nasri anakua mchezaji wanne kuondoka kwa mkopo Etihad Stadium kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, akitanguliwa na Wilfried Bony aliyejiunga na  klabu ya Stoke City, Joe Hart aliyeelekea nchini Italia kwenye klabu ya Torino pamoja na Eliaquim Mangala aliyekwenda Valencia ya Hispania.

Video: Popote pale haki isipotendeka hupelekea kutokea machafuko - Bisimba
Kevin Yondani Aondolewa Taifa Stars