Kuelekea maadhimisho ya wiki ya maji serikali inatarajia kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi ya maji 281 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.04.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Antony Sanga amesema maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika kuanzia machi 16 hadi  22 mwaka huu.

“Lengo la kufanya uzinduzi wa miradi hii katika kipindi cha wiki ya maji nikutumia fursa hiyo kuonyesha kwa vitendo mafanikio katika sekta ya maji na namna ambavyo huduma ya maji safi na usafi wa mazingira umeweza kuboreshwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi,” amesema Mhandisi Sanga.

Ameongeza kuwa wiki ya maji kutafanyika shughuli za upandaji wa miti katika vyanzo vya maji kuhabarisha na kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji .

Ambapo Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni “Thamani ya maji kwa uhai na maendeleo, ambayo itasaidia kusimamia rasilimali za pamoja na utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira nchini,”

Katibu mkuu huyo amewataka wananchi kutumia wiki ya maji kupata elimu namna bora ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kutoa changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

Familia ya Floyd kulipwa dola milioni 27
Mbaroni kwa uzushi juu ya afya ya Rais Magufuli