Serikali mkoani Dodoma imetangaza kuwa kuanzia Jumatatu tarehe 8 mwezi huu, miradi yake minne iliyojengwa na kukamilika katika jiji la Dodoma itaanza kutumiwa na wananchi.

Miradi hiyo ni stendi ya mabasi, soko, maegesho ya malori na eneo la mapumziko Chinangali, ambapo Serikali tayari imeagiza mabasi yote ya mikoani kuhamia katika stendi hiyo.

Zaidi ya shilingi bilioni 47 zimetumika kugharamia miradi hiyo tangu Rais Dkt. John Magufuli alipoitangaza Dodoma kuwa jiji.

Imeelezwa kuwa mchakato wa kuwapata waendeshaji katika soko kuu la Ndugai, Stendi Mpya ya mabasi, eneo la mapumziko Chinangali na maegesho ya malori Nala unaendelea.

Mbinu mpya kukabili madalali wa ufuta
Zahera: Sitaki kuifundisha Township Rollers