Misri imerejea tena katika kundi la mataifa 50 bora kwa soka duniani kwenye orodha ya Fifa ya mwezi Septemba.

Taifa hilo lilipanda hatua tatu na sasa limo nambari 49, hii ikiwa ni mara yao ya kwanza kwao kuwa katika 50 bora mwaka huu.

Mwaka 2014, walikuwa wamepanda hadi nambari 24 lakini wakaporomoka kutokana na kushindwa kwao kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.

Kwingineko, Rwanda ndiyo nchi pekee iliyopanda Zaidi ya hatua 10 duniani, baada ya kupanda hatua 13 na kutua nambari 78.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 59, Uganda imo nambari 74, Sudan 87, Ethiopia 99, Kenya 116, Burundi 132, Tanzania 140 na Sudan Kusini 195.

Duniani, Argentina bado inaongoza ikifuatwa na Ubelgiji, Ujerumani, Colombia na Brazil.

Mataifa bora ya Afrika kwa mujibu wa orodha hiyo mpya ya Fifa ndiyo haya, nambari iliyo kwenye mabano ikionyesha nambari kwa jumla duniani:

1 (19) Algeria

2 (21) Ivory Coast

3 (27) Ghana

4 (33) Tunisia

5 (38) Senegal

6 (42) Congo

7 (42) Cameroon

8 (49) Misri

9 (53) Nigeria

10 (56) Cape Verde

Wavuta Sigara Wamsaka Mshindi Messi Vs Ronaldo
Mke Wa Dk Slaa Amkana, Amwita Muongo