Misri imethibitisha kuwa na mgonjwa wa corona na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza barani Afrika kuripoti maambukizi hayo.

Msemaji kutoka Wizara ya Afya, Khaled Mugahed amesema Mgonjwa huyo ni Raia wa Kigeni na hakuonesha dalili zozote za kuwa na Virusi hivyo hapo awali ambapo amelazwa na yupo katika uangalizi maalumu.

Mgonjwa huyo ambaye Uraia wake haujawekwa wazi aligunduliwa kupitia programu maalum iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya Wasafiri wanaotoka nchi ambazo zimeripoti kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Hadi sasa, Ugonjwa wa COVID19 ambao husababishwa na virusi vya Corona, umesababisha vifo vya watu 1,400 na Idadi ya walioathirika imefikia 65,000.

Video: Tundu Lissu aibua mapya ughaibuni, PM: Msigeuze Corona kuwa mtaji wa kisiasa
Muumini mbaroni kwa kuiba sadaka kanisani

Comments

comments