Muigizaji wa filamu za kibongo Chuchu Hans ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanga mwaka 2005 amefunguka kuhusu kusimamia shindano la Miss Tanga ambapo amesema kuwa anatumia jina lake ili kukuza vipaji kwa vijana.

Amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa amejipanga kufanya tamasha hilo kwa kufuata taratibu zilizowekwa katika kuandaa mashindo ya mamisi na kwamba miss Tanga itakuwa ya tofauti.

Aidha, amesema wadhamini wanatakiwa kurudisha tena imani yao katika kuandaa matamasha kwani baada ya mashindano haya kuzorota na wao wakapotea, ameongeza kuwa wadhamini ni muda wao kurejea na kuunga mkono mashindano haya kwani Miss tanga ameandaa mwenyewe.

Faida 7 za kula tango
Uwanja wa ndege Saudi Arabia washambuliwa na waasi

Comments

comments