Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana iliwapunguzia mzigo wa mashtaka, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Harry Kitilya

Harry Kitilya

Mahakama hiyo imewafutia watuhumiwa hao shtaka zito la utakatishaji fedha (money laundering) lililokuwa kati ya makosa matatu yaliyokuwa yakiwakabiri. Mashtaka mengine yanayowakabili ni pamoja na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu pamoja na kugushi nyaraka.

Katika kesi msingi, watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa kosa la kufanya udanganyifu na kujipatia kiasi cha dola milioni 6, kama malipo ya kuisaidia serikali kupata mkopo wa dola milioni 550 (zaidi ya trilioni 1.3) kutoka Benki ya Stanbic tawi la Londoni Uingereza, kupitia Stanbic tawi la Dar es Salaam. Madai ambayo watuhumiwa wote waliyakana.

Dele Alli Aingia Kwenye Kitanzi Cha FA
Arsene Wenger Kuifumua Safu Ya Kiungo Na Kuifuma Upya