Serikali ipo katika mchakato wa kupitia upya mitaala ya elimu nchini ili kuendana na hali ya sasa.

Kamishna msaidizi Kitengo cha Kinga na Huduma za Jamii wa DCEA Moza Makumbuli amedokeza kuwa tayari Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,imeshirikishwa katika mchakato huo kwa kutoa mapendekezo yao ili utoaji elimu kuhusu dawa za kulevya uwepo kwenye mitaala ya shule za msingi na sekondari

Utoaji elimu kuhusu dawa za kulevya mashuleni ni kati ya vipaumbele vya mamlaka hiyo katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini,ambapo DCEA imependekeza serikali kupitia kwa wizara ya elimu, kurasimisha mpango huo kwa kuuweka kwenye mitaala.

Serikali yazindua mkakati wa kutokomeza ukeketaji
Watatu warejea Simba SC