Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ametangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita Juni 29 na kukamilika Julai 16, 2020.

Aidha ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kusambaza mitihani mara moja, lakini pia kuhakikikisha matokeo yanatoka kabla ya Agosti 30, mwaka huu.

Waziri Ndalichako amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Vyuo Vikuu ipo tayari bodi hiyo ina fedha kiasi cha sh.bilioni 122.8 kwa ajili ya wanafunzi wenye sifa ya kupata mikopo hiyo.

Aidha amesema kwa sasa vyuo vinatakiwa kuwasilisha nyaraka hadi Mei 28, 2020 ziwe zimefika bodi ya mikopo ili itoe fedha hizo kwa wanafunzi watakapofika vyuoni.

Bendera ya Marekani yashushwa nusu mlingoti, maombolezo vifo vya corona
Kante ahofia mazoezi Chelsea