Maneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Njombe, Gasper Matiku amezitaka Hospitali Mbalimbali mkoani humo kuhakikisha kuwa mizani wanayoitumia katika shughuli zao za matibabu Zinafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara ili kuepuka mizani hiyo kudanganya katika utoaji taarifa za Wagonjwa na kuathiri matibabu yao.

Ikiwa ni Wiki ya Vipimo Duniani wakala wa Vipimo Mkoani Njombe wametembelea na kufanya ukaguzi katika Hospital ya Rufaa Kibena pamoja na Kituo cha afya Njombe Mjini ambapo wamebaini kuwapo kwa mizani 14 yenye changamoto kati ya 26 iliyokaguliwa.

Aidha, mara baada ya kubaini kuwepo kwa mizani yenye changamoto Maneja wa Wakala wa Vipimo amezitaka Hospital na Vituo vya afya pamoja na Zahanati kuwa na utaratibu wa kutenga fedha kwaajiri ya matengenezo ya Mizani hiyo pindi ikiharibiki.

“Kwa hiyo tunawashauri ni vizuri sasa wakatenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya kuona hizi mizani zisitumike tu bila kufanya service kwa sababu mizani ni kama mashine inavyotumika usahihi wake unaweza kupotea, kwasababu kuna sehemu ambazo kulingana na matumizi zinakuwa zinalika,”amesema Matiku

 

Nyota wa Stars hoi kitandani, TFF, Shirika la Posta watupiwa lawama kwa kumterekeza
Video: Watumishi wote ardhi Moro kuhamishwa | Kashfa nzito Hospitali