Sakata la wabunge wa Upinzani kutaka kumuondoa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson limepata nafasi ya kuanza kuzungumziwa leo Bungeni ikiwa ni siku chache baada ya upande wa Upinzani kuwasilisha rasmi kusudio lao.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah amesema kuwa leo atalielezea suala hilo baada ya kujiridhisha kuhusu taratibu na hatua zinazopaswa kufuatwa.

“Nitaeleza kinachoendelea kesho (leo) baada ya kujiridhisha kuhusu taratibu zinazopaswa kufuatwa kuhusu suala hilo,” Dk. Kashillilah alisema.

Kambi rasmi ya upinzani imekuwa ikisusia vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa lengo la kushinikiza aondolewe katika kiti hicho.

Wiki iliyopita, Kambi hiyo kupitia kwa Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya iliwasilisha rasmi kusudio lao la kumuondoa Naibu Spika kwa kuwa hawana imani naye huku wakiainisha sababu sita zinazopelekea uamuzi huo.

Walizitaja sababu hizo kuwa ni upendeleo kwa wabunge wa CCM, kusimamia maslahi ya Serikali badala ya umma, kutokuwa mwanasiasa, jambo linalomfanya akose uzoefu wa kuendesha vikao vya Bunge, ubabe, unyanyasaji kwa wabunge wa upinzani na kusimamia fedha za Mfuko wa Bunge zirudishwe kwa Rais.

Arsenal Kuibomoa Leicester City, Wamtaka Riyad Mahrez
TFF Yapangua Kamati, Wakili Komba Apewa Kamati Ya Rufani Ya Nidhamu