Mama mjane anayefahamika kwa jina la Etinala Magehema maarufu kwa jina la Manyanye mkazi wa mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya mji wa Njombe ametoa wito kwa vijana na akina mama kuto kukata tamaa na maisha badala yake kuongeza juhudi katika kufanya kazi yoyote.

Akizungumza na Dar24 amesema kuwa katika maisha yake amefanikiwa kwa kiasi kutokana na kuuza Viazi, Uji, Chai na Makande magerejini huku akihifadhi anachokipata na kumuwezesha kujenga nyumba ya kuishi na familia yake.

“Nyumba yangu nilianza kujenga kwa kuuza Kande na Viazi vya kuchoma magerejini wakiwa watu hawaelewi hapa Njombe na mimi nikiwa nimeanza bila wengine kuijua biashara hiyo kwenye miaka ya 2000, nimeuza mpaka miwa huku zile hela nikicheza mchezo mpaka nikanunua uwanja na kipindi hicho mume wangu alikuwa ana nguvu akanisaidia kujenga” alisema Manyanye.

Mama huyo ambaye kwa sasa anaishi na watoto saba katika nyumba yake aliongeza kuwa kwa sasa anajishughulisha na kazi ya ugongaji kokoto licha ya kuwa na umri mkubwa bila kukata tamaa na amefanikiwa kunza kujenga nyumba nyingine ambayo imefikia katika hatua ya msingi.

Ametoa wito kwa vijana wenye nguvu kuto kubweteka huku akiwaomba mabinti walio kwenye ndoa kuacha kutegemea mwanaume badala yake kujishughulisha ili kusaidiana katika familia.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 19, 2019
Kodak black achafua hali ya hewa kwa mashabiki, Polisi waingilia kati