Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amezindua WiFi ya mtandao wa  bure katika chuo cha elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam, na kuwaomba wanafunzi wa chuo hicho kuitumia WiFi hiyo kwa tija ya masomo ikiwemo kufanya tafiti mbalimbali zitakazo wasaidia katika masomo yao na jamii kwa ujumla.

Mjema ameupongeza mradi huo wa WiFi ya bure ambao unaendeshwa na kampuni ya Tanzanite Technology Co. Ltd kwa kushirikiana na manispaa ya Ilala na kampuni ya simu ya TTCL kwani unatarajia kuwanufaisha zaidi ya watumiaji 7000 ambao ni wahadhili, wafanyakazi, wanachuo na wadau mbalimbali.

Huku lengo kubwa likiwa ni kujenga daraja la Teknolojia na kuondoa pengo kati ya walio na uwezo wa kutumia mtandao wa Internet na wasio kuwa na uwezo, ambapo Mjema amesisitiza endapo kutakuwa na matumizi sahihi ya Teknolojia hiyo taifa kwa ujumla litapiga hatua na ufaulu kuongozeka kwa wanafunzi nchini.

Live: Waziri Mkuu wa Ethiopia awasili Tanzania
Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela kwa Kughushi Cheti

Comments

comments