Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Jan Kubis, amejiuzulu wadhifa wake mwezi mmoja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi katika taifa hilo lililogawika na vita.

Kubis amejiuzulu bila ya kutoa sababu kwa wanachama wa baraza la Usalama juu ya uamuzi wake.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema Guterres anaendelea na mchakato wa kujaza nafasi hiyo.

Kubis, mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mjumbe wa zamani wa Umoja wa Mataifa kwa Lebanon, alichukua nafasi hiyo ya Libya mnamo mwezi Januari.

Uchaguzi wa kwanza wa Urais nchini Libya unatarajiwa kufanyika Disemba 24, wakati Umoja wa Mataifa unajaribu kumaliza mgogoro wa muongo mmoja tangu kuondolewa kwa kanali Moammar Gadafi mnamo mwaka 2011.

Waziri Mkenda awasili Uganda kwa ziara ya siku tatu
Jay Z ajiandikia rekodi ya kipekee tuzo za Grammy