Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokraasia na Maendeleo (CHADEMA), Muslim Hassanali aliyekuwa mgombea ubunge mwaka 2015 amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM.

Kujiunga kwa Muslim Chama cha Mapinduzi ni muendelezo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge kukihama chama hicho.

Aidha, viongozi kadhaa wa upinzani wamekuwa wakihama vyama vyao na kujiunga na chama tawala kwa lengo la kuunga mkono juhudi za rais Dkt. Magufuli za kupambana na rushwa.

Hata hivyo, kiongozi huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, huku Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole akisema kuwa Muslim amekuwa akiomba kujiunga na CCM kwa muda mrefu.

Mtulia atii agizo la CCM
Chid Benz atiwa mbaroni kwa mara nyingine