Kiungo Frank Lampard huenda akaitema ofa ya klabu yake ya zamani ya Chelsea, ambayo ilionyesha kuwa tayari kumpokea na kumpa jukumu la kuwa sehemu ya benchi la ufundi.

Lampard ameanza kuhisiwa huenda akaitema ofa hiyo, kutokana na ofa nyingine kubwa iliyotoleawa na klabu ya MK Dons inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Chelsea bado wanasubiri majibu ya Lampard, baada ya kuwasilisha pendekezo lao kwake, saa chache baada ya kuthibitishiwa hatosaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya New York City FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani (MLS).

Kwa upande wa MK Dons wamedhamiria kumpa ajira Lampard kwa kuamini ataweza kukinusuru kikosi chao kutokushuka daraja, huku wakitegemea sana uzoefu wake wa kucheza soka pamoja na uhamasishaji.

Kwa sasa klabu ya MK Dons inanolewa na meneja wa mpito Richie Barker, baada ya kutimuliwa kwa Karl Robinson mwezi Oktoba mwaka huu.

Video: Waziri atoa onyo kwa wakuu wa mikoa, ni kuhusu madawati
Liverpool, Celtic, Newcastle Utd Zamuwania Steven Gerrard