Wataalam wa Afya kanda ya Kaskazini, inayounda mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Tanga wameweka maazimio ya pamoja yatakayorahisisha kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

Wakitoa maazimio hayo, baadhi ya wataalam hao akiwemo Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga, Raphael Mumba, Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Mount Meru, Sinpho Siale na Daktari Bingwa magonjwa ya mama na uzazi hospitali ya Rufaa Kilimanjaro-KCMC, Dkt.Glory Mangi wamesema lengo la maazimio hayo ni kupunguza vifo.

Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Kaskazini, Haikamesia Malisa amesema maazimio ya kikao hicho cha siku mbili yatakuwa ni kipimo kwa kila robo mwaka cha utekelezaji, huku mwakilishi wa Mganga Mkuu mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Andrewleon Saashisha Quaker akisema watatekeleza maazimio hayo.

Afisa Programu  Wizara ya Afya, Idara ya Afya ya Uzazi, mama na Mtoto, Jackline Ndanshau amesema ni muhimu kutekeleza maazimio  hayo.

Vikosi vya usalama vyawasili katika mpaka na DRC
Jean Baleke amtaja Moses Phiri, Chama