Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeiraumu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuchomeka vipengere viwili kikiwemo kile kinachoweka masharti magumu dhidi ya sifa ya mgombea wa urais wa chama hicho.

Vipengere hivyo vinadaiwa kuchomekwa kwenye kanuni namba nane ya uchaguzi ya TLS katika toleo la serikali namba II6 la mwaka 2018.

Kipengere kinacholalamikiwa na TLS kinachodaiwa ni mkakati wa kumng’oa Lissu ni kile cha nane (e) ambacho kinasema mgombea yeyote wa urais ambaye atakuwa ni mtumishi wa umma, mbunge, diwani au nafasi yeyote ya uongozi ndani ya chama hataruhusiwa kugombea uraisi ndani ya chama hicho cha wanasheria.

Aidha, vipengere hivyo tayari vimeibua mijadala na hisia kubwa ndani ya chama cha wanasheria Tanganyika TLS wengi wakidai kuwa hilo ni kusudio la kumuengua rais wa sasa wa chama hicho Tundu Lissu.

“Ni kweli kabisa kanuni tuliyoiandaa imechomekewa kipengele ambacho hakikuwapo kabisa, sisi tulitengeneza kanuni ambayo kimsingi tulikuwa tunairekebisha ile ya mwaka 2016,”amesema Makamu wa Rais wa chama hicho Godwin Ngwilimi

Hata hivyo, wakili wa kujitegemea, Thomas Msasa amesema kuwa mabadiliko hayo ya kanuni walipatiwa kwa njia ya barua pepe, Februari 14.

Manny Pacquiao amtaja mpinzani wake pambano lijalo
Mamlaka ya Hali ya Hewa yatoa tahadhari na angalizo kwa wananchi