Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Jijini New York nchini Marekani.

Dkt. Mpango yupo nchini humo kumwakilisha Rais Samia na leo (Septemba 22, 2022 majira ya saa nne usiku), anatarajia kuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA), unaondelea.

Tayari Viongozi kadhaa wametoa hotuba zao akiwemo Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, Rais wa Senegal, Macky Sall, Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Kenya, William Ruto.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro unaopatikana nchini Tanzania Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, nchini Marekani.
Dkt. Philip Mpango na Antonio Guterres.
Serikali yawageukia Wafanyabiashara wa Mkaa
JMKF yaandaa mafunzo uwezo wa kujiamini kwa Watoto wa kike