Mzaha na mbinu chafu za kutaka kuwashinda mahasimu wake zimemponza kiongozi wa G- Unit, 50 Cent ambaye anaripotiwa kuwa katika hali mbaya kiuchumi huku akitangaza kufilisika.

Ukata huo wa 50 Cent umetokana uamuzi wa kisheria wa mahakama iliyomtia hatiani kwa kosa la kuvujisha makusudi mkanda wa ngono ambao mama mtoto wa Rick Ross alishiriki. Imeelezwa kuwa 50 aliamua kuvujisha mkanda huo kwa lengo la kumuudhi na kumuaibisha hasimu wake Rick Ross.

Kwa mujibu wa TMZ, mahakama iliamua 50 Cent amlipe Lavonia fidia ya dola milioni 5 ($5 million).
50 ameangukia pua katika kesi nyingine ya kudokoa ubunifu wa mtindo wa headphones. Baada ya kumkuta na hatia, Jumba la Polato hao wa Marekani lilimtupia mzigo wa kulipa fidia ya dola milioni 17.2.

Kwa mujibu wa page 6, 50 ailitaka mahakama hiyo itambue kuwa anatangaza mufilisi (amefilisika) kwa kuwa kuna ulinganifu kati ya madeni na mali anazomiliki.

Mahakama hiyo imemtaka rapa huyo kupeleka vielelezo ili kiasi cha pesa alizopigwa faini kiweze kufikiriwa.
Miezi iliyopita, jarida la Forbes lilionesha makadilio ya utajiri wa 50 Cent kuwa dola milioni 115. Hii inaonesha kuwa fedha sio rafiki wa kudumu.

Hata hivyo, 50 Cent ameomba kutangazwa mufilisi inayoitwa ‘Chapter 11 bankruptcy’.

Hii ndio maana ya Chapter 11 bankruptcy kwa mujibu wa tovuti ya mahakama ya Marekani:

“This chapter of the Bankruptcy Code generally provides for reorganization, usually involving a corporation or partnership. A chapter 11 debtor usually proposes a plan of reorganization to keep its business alive and pay creditors over time. People in business or individuals can also seek relief in chapter 11.”

Babu Hans Apangua Upya Kikosi Cha Yanga
Raila Odinga Aeleza Kenya Ilivyopokea Ushindi Wa Magufuli Na Kama Aliwahi Kumgusia Kuutaka Urais