Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amewasili wilayani Chato kwa ajili ya kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa afya wilayani humo.

Makabidhiano hayo yanafanyika kwa niaba ya mikoa mingine mitatu ambayo pia imejengewa nyumba hizo na Taasisi ya Benjamin Mkapa

Naye Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida ataungana na Rais Mkapa kukabidhi mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti. Mtambo huo umejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, kama ambavyo taarifa ilivyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa tasisi hiyo, Richard Bagolele.

Kesho, Rais John Magufuli ambaye yupo mapumziko wilayani Chato, atashiriki katika hafla ya makabidhiano hayo yatakayofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu Chato.

Video: Majaliwa awahakikishia wawekezaji mafanikio
Mourinho atoa maneno ya busara kumuaga Rooney