Serikali ya Tanzania imetengaza siku tatu mfululizo za kuaga mwili wa rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Julai 24, 2020.

Akitangaza ratiba ya maombolezo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba Watanzania watapata fursa ya kuuaga mwili wa Hayati Mkapa kuanzia Jumapili Julai 26 hadi Jumanne ijayo Julai 28.

“Kanisa la Roman Catholic ndilo wataendesha ibada ya maombolezo siku ya Jumapili pale Taifa, kuaga itakua siku nzima kwa siku zote tatu.

“Jumanne itafanyika ibada ya Kitaifa, viongozi mbali mbali na watumishi wa Umma watapata fursa ya kuaga kuanzia asubuhi hadi saa sita mchana, na saa nane utasafirishwa kwenda Kijiji kwao Lupaso.” amesema Majaliwa

Amesema siku ya Jumatano Julai 29 wakazi wa Mtwara na vitongoji vyake watapata fursa za kuaga mwili wa Mzee Mkapa na saa nane kamili atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Majaliwa amesema katika kipindi hiki dunia inapambana na janga la Corona, kiongozi kutoka nchi za nje atakaependa kushiriki basi ubalozi wa nchi zao utoe tarifa ili mazingira mazuri ya kuwawezesha kushiriki yaandaliwe.

Mabalozi wafika nyumbani kwa Mkapa kuomboleza
Kocha Sven akubali kiwango Simba SC