Wakala wa beki wa kulia kutoka nchini Hispania Hector Bellerin, amesema mchezaji huyo anakaribia kusaini mkataba mpya na uongozi wa klabu ya Arsenal.

Albert Botines ambaye ni wakala wa beki huyo, amesema mpaka sasa hatua waliyofikia ni nzuri na anaamini wakati wowote kabla ya mwaka mpya, hatua ya kusainiwa mkataba mpya itakamilishwa.

Bellerin, alianza mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, baada ya kukataa mpango wa kurejea FC Barcelona ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dani laves alietimkia Juventus FC.

Bellerin, alijiunga na Arsenal mwaka 2011 akitokea FC Barcelona ambapa walikubali kumuachia kama sehemu ya dili la usajili wa kiungo Cesc Fabregas.

“Tumezungumza na tumefikia pazuri, nina uhakika wakati wowote mambo yatakua sawa,” alisema Botines alipozungumza na Sky Sports.

“Hector amekua na maisha ya furaha akiwa hapa (Arsenal), amenihakikishia suala hilo, na ndio maana alikataa kurejea FC Barcelona.”

Safari Za Timu Zote Za Taifa
TFF: Young Africans Vs Ruvu Shooting Kupigwa Kesho