Wananchi wa Zimbabwe wameiangukia Serikali wakiitaka itafute suluhu ya mgogoro wa kiuchumi unaoikabili nchi hiyo, kutokana na kupanda mara mbili kwa bei ya mkate.

Kwa mujibu wa Reuters, Jumanne wiki hii bei ya mkate iliyokuwa juu ilipanda mara dufu hadi kufikia 3.50 RTGS dollars kutoka 1.80 ya awali kwa maduka mengi yaliyotembelewa.

“Mkate umekuwa chakula cha anasa. Ni watu wangapi hapa wanaweza kumudu gharama hiyo y amkate,” Reuters wanamkariri Sarah Chisvo, mama wa watoto watatu ambaye anafanya kazi kwenye mgahawa wa chakula jijini Harare.

“Tunaiomba Serikali kuingilia kati na kutusaidia hasa sisi wanyonge kabla mambo hayajatuzidia,” aliongeza mama huyo.

Februari mwaka huu, Zimbabwe iliamua kuanzisha fedha yake ya dharura kwa ajili ya kusaidia anguko la thamani ya fedha dhidi ya Dola ya Marekani. Waliita Real Time Gross Settlement dollar (RTGS). Hata hivyo, imezidi kushuka thamani tangu wakati huo na kusababisha makampuni kupandisha bei za bidhaa zao.

Zimbabwe iliathiriwa na ukame katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo. Hali hiyo ilisababisha kulazimika kutumia fedha zake chache za kigeni kununua vyakula kutoka nchi za jirani.

Serikali ya Uganda yafikiria kumpa hifadhi Al-Bashir
Mwanafunzi afariki dunia akipiga picha na wenzake