Mahakama ya Rufaa nchini Sudan imebadili hukumu ya kifo dhidi ya mwanamke ambaye alimuua mume wake kwa madai kuwa alimbaka.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 aliyetajwa kwa jina la Noura Hussein, alikuwa amehukumiwa kifo lakini mahakama hiyo imeamua atumikie kifungo cha miaka mitano jela, kwa mujibu wa mwanasheria wake Abdelaha Mohamad.

Mama yake, Zainab Ahmed amesema kuwa amefurahishwa na madiliko ya hukumu hiyo na kwamba mwanaye atamuona tena.

Watu maarufu duniani kote waliifanya kampeni ya yenye hashtag #JusticeforNoura, inayolenga kumsaidia Noura apate haki yake, hali iliyoibua watu wengi zaidi kuiunga mkono.

Mwezi uliopita, Mahakama inayofuata sheria kali ya kidini ilimhumuku kufa kwa kunyongwa, baada ya kumkuta na hatia ya kumuua mumewe Abdulrahman Mohamed Hammad.

Katika maelezo yake mahakamani, mwanamke huyo alisema kuwa mumewe aliwatumia binamu zake wa kiume kumshika na kumlaza chini wakati akimbaka.

Alieleza kuwa mwanaume huyo alipojaribu kumbaka tena siku iliyofuata, alimponyoka na kuchukua kisu kisha kumchoma hadi kufa.

Hawa ndio viongozi wadaiwa sugu JWTZ
Rais wa Zimbabwe ataja kundi la Mke wa Mugabe kutaka kumuua