Mke wa Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Grace Gwajima mapema leo ameambatana na mume wake katika tukio la kuzungumza na vyombo vya habari kufuatia sakata linalosemekana kuwa video za mume wake akiwa faragha kuvuja mitandaoni.

Mke wa Gwajima ametoa msimamo wake na kusema kuwa anamuamini mume wake na ameahidi kusimama naye katika kipindi hiki kigumu cha majaribu anachokipitia

Amesema ”Ukweli ninaufahamu, Mume wangu ninamfahamu na ninamwamini na ukweli huo hakuna mtu anayeweza kuubadilisha nipo pamoja na yeye nitasimama na yeye na Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayeweza kuwa juu yetu” amesema mke wa Askofu Josephat Gwajima.

Ameongezea kuwa ”Wouvu hukimbia bila hata kufuatwa na mtu na wenye haki ni jasiri kama simba mimi ni jasiri kama simba”.

Mke wa Gwajima amesema hayo mara baada ya mume wake kuzungumza mbele ya vyombo vya habari akiwa kanisani kwake ubungo baada ya video ambazo zimesambaa mtaondoni na kusema kuwa mtu aliye katika video hiyo si yeye bali ni picha zimeungwa ungwa na kuonesha kuwa ni yeye.

Hivyo amemtaka aliyehusika na kumchafua afanye kile kinachotakiwa kufanya kwani tayari hatua kisheria zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kukata RB kwa yule aliyevujisha video hiyo mtandaoni.

VIDEO: Askofu Gwajima ni MUATHIRIKA siyo MTUHUMIWA - Mambosasa
LIVE: MWILI WA DKT. MENGI UKIWASILI KILIMANJARO MUDA HUU