Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change kimelitaka jeshi la polisi kumkamata mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe, mama Grace kwa sakata la kutunukiwa Shahada ya Uzimivu (PhD) bila kutimiza vigezo stahiki.

Inadaiwa kuwa Mama Grace alifanikiwa kutunikiwa PhD ndani ya miezi michache kinyume cha taratibu za kiwango hicho cha elimu ambapo mtu anapaswa kusoma kwa miaka kadhaa.

Kamati ya Kupambana na Rushwa iliyofanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo imesema imemkamata Profesa Claude Mararike aliyesimamia utafiti wa Mama Grace uliosaidia kutimiza kigezo muhimu cha kutunikiwa PhD.

Kamati hiyo pia imemkamata Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Levi Nyagura kufuatia sakata hilo.

Hata hivyo, kamati hiyo pamoja na Jeshi la polisi wamesisitiza kuwa Mama Grace hastahili kukamatwa kwani yeye alikuwa mwanafunzi ambaye hakujua taratibu za kukamilisha vigezo vya kutunukiwa PhD, utaratibu ambao alipaswa kuelezwa na Chuo Kikuu cha Zimbabwe.

Grace alitunukiwa PhD yake kutoka Chuo Kikuu hicho mwaka 2014 na wasiwasi wa kuwa alipendelewa ulianza kwa kuunganisha nukta kuwa mumewe alikuwa Rais na Mkuu wa chuo hicho.

Pia, ilielezwa kuwa hakutumia muda mwingi kuwa shuleni wakati huo kutokana na kuonekana kwenye amejikita kwenye majukwaa ya harakati za kurithi kiti cha mumewe.

Chuo Kikuu cha Zimbabwe kililazimika kuweka kwenye tovuti yake utafiti ambao unaaminika ulifanywa na Mama Grace.

Ngorongoro Heroes, Twiga Stars kusaka nafasi Afrika
Video: Mbowe awataja waliomtuma Musiba