Mke wa marehemu Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto amesema kuwa amefukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mume wake jijini Tanga maeneo la Donge.

Amesema kuwa watoto wa marehemu pamoja na Ndugu wa Mzee Majuto ‘wamemfukuza’ wakidai kuwa hawana pesa za kumsaidia hivyo ajisaidie mwenyewe kupitia pesa za pole anazopata toka kwa watu.

”Toka amekufa marehemu mume wangu hakuna mtu yeyote amenisaidia zaidi ya Watanzania na marafiki wa marehemu” amesema mke wa Majuto.

Yapata siku 12 tangu mwigizaji Mzee Majuto afariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mke wake ambae walizaa watoto wanne ameongea na chombo cha habari cha Ayo TV nakuomba msaada toka kwa watanzania wamsaidie kwani sasa yupo eda na hana msaada wowote.

”Mimi mpaka dakika hii atakayeweza kunisaidia kwa chochote kile nipo tayari iwe kimawazo, kipesa, kibiashara nipo tayari” amesema Mke wa Majuto.

Amesema kwamba alipokuwa anaishi na mume wake mkoani Tanga amefukuzwa na sasa anasaidiwa na ndugu zake anapatikana jijini Dar es salaam maeneo ya Vingunguti machinjioni.

Diva aomba kuchangiwa Dola 7000 kujitibu, 'Nimelia sana'
Breaking: Basi lililobeba abiria 60 lateketea kwa moto Kigoma